BIBLIA (Cross_Small-Size)

11,500.00Fr

KWA MSOMAJI,
Hii ndiyo tafsiri mpya ya Neno la Mungu katika lugha ya Kiswahili, nayo imefanywa kwa matumizi ya Wakristo wa Kanisa la Mungu katika nchi zote kunakosemwa Kiswahili. Tafsiri nyingi za Kiswahili zilizo mbalimbali zimefanywa siku zilizopita, za Agano la Kale, na za Agano Jipya. Tunawashukuru sana watu hao waliofanya tafsiri hizi tunazozipenda, ambazo kwa hizo tumepata baraka kuu za kiroho.
Lakini haiwezekani kwamba watu wa British and Foreign Bible Society,huko London, waendelee kupiga chapa Biblia katika msemo wa Kiswahili cha Kimvita na cha Kiunguja, na Jumuiya nyinginezo kupiga chapa tafsiri nyingine nyingine;basi imedhaniwa ya kwamba roho ya umoja itazidi kuonekana katika Kanisa la Mungu kila mahali katika Afrika ya Mashariki kama ikiwezekana sote tuwe na namna moja ya Biblia katika Kiswahili. Basi tafsiri hii mpya ilipoanza kutengenezwa ilitupasa kuchagua na kuyatumia yote yaliyokuwa mema zaidi katika tafsiri za zamani, ili kufanya kitabu kimoja kipya. Kazi hii imeendelea sasa kwa miaka mingi, na hao wenye kutafsiri wamesaidiwa katika kazi yao na watenda-kazi wenzi wao wengi, Wazungu kwa Waafrika, pande zote za Afrika Mashariki. Zaidi ya yote tumejua ya kwamba Mungu Roho Mtakatifu ametuongoza na kutusaidia katika kazi hii, nasi twatumaini sana ya kwamba,kwa nguvu za Roho yeye yule, tafsiri hii nayo itawaletea baraka kuu wote waisomao.

Hapana budi wasomaji wengine wataona ya kwamba kuna mageuzi ambayo kwanza hawatayapenda, hili ni lazima kwa Wakristo wa kila mahali, ambao wamezoea vitabu vyao vya zamani. Pamoja na hayo, pengine maneno hayo watakayoyakataa watu wasemao Kimvita siyo yale watakayoyakataa wanaotumia Kiunguja. Basi, na tukumbuke sote kila tutakapokisoma kitabu hiki, ya kwamba wenye kufanya kazi hiyo wamejaribu sana kutafsiri Neno la Mungu katika lugha itakayowaelea wote. Wala isidhaniwe kabisa kwamba katika tafsiri hii kuna mageuzi yo yote yaliyofanywa ya Neno la Mungu.Hasha!Jambo hilo haliwezekani kabisa. Lakini, na tukumbuke ya kwamba Neno la Mungu halikuandikwa kwanza kwa lugha ya Kiingereza, wala ya Kiswahili.Roho Mtakatifu aliwavuvia watu watakatifu wa kale, Wayahudi na Wakristo,ili kudhihirisha na kutangaza Neno la Mungu. Hao Wayahudi wakatuandikia Neno hilo kwa lugha ya Kiebrania, katika Agano la Kale, tena hao Wakristo wakaliandika kwa Kiyunani, katika Agano Jipya. Basi watu wanaotafsiri Biblia katika lugha za sasa, kwanza huangalia kwa kutunza sana maneno hayo ya asili yaliyoandikwa zamani kwa lugha ya Kiebrania na Kiyunani; kisha wakajaribu kuandika tafsiri iliyo halisi. Mara kwa mara inawezekana kutengeza kidogo hizo tafsiri zilizotangulia kufasiriwa, nasi tumejaribu kufanya hivi, pamoja na kuungamanisha hizo tafsiri za kale.

Category:

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “BIBLIA (Cross_Small-Size)”

Your email address will not be published. Required fields are marked *