BIBLIA (Medium-Size)

11,500.00Fr

DIBAJI

Tafsiri hii mpya ya Kiswahili imefanyika kwa ushirikiano wa makanisa ya Kikristo,Wakatoliki kwa Waprotestanti, pamoja na Vyama vya Biblia.
Hii tafsiri ya pamoja ilianzishwa katika mwaka wa 1973, wakati ambapo Wakristo wengi wa Afrika Mashariki ambao Kiswahili ni lugha yao ya mawasiliano, walikwisha kuwa na hamu kubwa ya kuwa na tafsiri ya Biblia kwa Kiswahili chenye kueleweka vizuri zaidi kadiri ya matumizi ya msamiati wa sasa wa lugha yao. Ndiyo maana makanisa yakavitaka Vyama vya Biblia na Muungano wa Vyama vya Biblia vishughulikie jambo hilo.
Mojawapo ya mambo ya kimsingi yaliyozingatiwa katika tafsiri hii ni kwamba Mungu huongea na watu akitumia lugha yao wenyewe na msamiati uleule wanaoutumia wakati huo katika mawasiliano yao. Hali kadhalika,Mungu anapoongea nasi atatumia msamiati wa Kiswahili tunaoutumia sisi wenyewe. Hangetumia Kiswahili kilichoyumbishwa na Kigiriki au Kiebrania kama zilivyo tafsiri za neno kwa neno badala ya maana kwa maana.
Shabaha ya tafsiri hii siyo kuchukua nafasi ya tafsiri nyingine yoyote ya zamani ya Kiswahili. Shabaha yake ni kuwapatia watu tafsiri aminifu iliyo wazi na ambayo imetia maanani mapato ya kitaalamu ya siku za karibuni juu ya lugha ya Kigiriki (AJ) na Kiebrania au Kiaramu (AK) kama zilivyotumiwa nyakati za maandishi hayo; tafsiri iliyo katika muundo wa matumizi ya kila siku ya lugha ya Kiswahili nyakati hizi zetu.
Makala zilizotumiwa kutoa tafsiri hii ni Biblia Hebraica Stuttgartensia,1987,kwa Agano la Kale; na kwa Agano Jipya ni The Greek New Testament,iliyochapishwa na Muungano wa Vyama vya Biblia (toleo la 3 mwaka 1975).

Miswada ya tafsiri hii ilipelekwa kuhakikiwa na kusahihishwa na Kamati ya Uchunguzi wa Maandishi ambayo wajumbe wake, wataalamu kwa fani zao zinazohusika katika kazi ya namna hii, walikuwa wa makanisa mbalimbali.Nakala hizo pia zilipelekwa kwa viongozi wa makanisa, vyuo vya filosofia na theologia katika Kenya na Tanzania.
Wote waliohusika kwa mali na hali au kwa namna nyingine katika mradi huu tunawatakia baraka za Mwenyezi-Mungu.
Ilani kwa Msomaji: Maneno yaliyotiwa katika mibano mraba […]yanafikiriwa kuwa hayapatikani katika nakala zote za awali za Maandiko Matakatifu.

Category:

Description

HABARI NJEMA KWA WATU WOTE

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “BIBLIA (Medium-Size)”

Your email address will not be published. Required fields are marked *