Shop
Showing 25–36 of 46 results
-
BIBLIA (lux)
15,000.00FrKWA MSOMAJI,
Hii ndiyo tafsiri mpya ya Neno la Mungu katika lugha ya Kiswahili, nayo imefanywa kwa matumizi ya Wakristo wa Kanisa la Mungu katika nchi zote kunakosemwa Kiswahili. Tafsiri nyingi za Kiswahili zilizo mbalimbali zimefanywa siku zilizopita, za Agano la Kale, na za Agano Jipya. Tunawashukuru sana watu hao waliofanya tafsiri hizi tunazozipenda, ambazo kwa hizo tumepata baraka kuu za kiroho.
Lakini haiwezekani kwamba watu wa British and Foreign Bible Society,huko London, waendelee kupiga chapa Biblia katika msemo wa Kiswahili cha Kimvita na cha Kiunguja, na Jumuiya nyinginezo kupiga chapa tafsiri nyingine nyingine;basi imedhaniwa ya kwamba roho ya umoja itazidi kuonekana katika Kanisa la Mungu kila mahali katika Afrika ya Mashariki kama ikiwezekana sote tuwe na namna moja ya Biblia katika Kiswahili. Basi tafsiri hii mpya ilipoanza kutengenezwa ilitupasa kuchagua na kuyatumia yote yaliyokuwa mema zaidi katika tafsiri za zamani, ili kufanya kitabu kimoja kipya. Kazi hii imeendelea sasa kwa miaka mingi, na hao wenye kutafsiri wamesaidiwa katika kazi yao na watenda-kazi wenzi wao wengi, Wazungu kwa Waafrika, pande zote za Afrika Mashariki. Zaidi ya yote tumejua ya kwamba Mungu Roho Mtakatifu ametuongoza na kutusaidia katika kazi hii, nasi twatumaini sana ya kwamba,kwa nguvu za Roho yeye yule, tafsiri hii nayo itawaletea baraka kuu wote waisomao.
Hapana budi wasomaji wengine wataona ya kwamba kuna mageuzi ambayo kwanza hawatayapenda, hili ni lazima kwa Wakristo wa kila mahali, ambao wamezoea vitabu vyao vya zamani. Pamoja na hayo, pengine maneno hayo watakayoyakataa watu wasemao Kimvita siyo yale watakayoyakataa wanaotumia Kiunguja. Basi, na tukumbuke sote kila tutakapokisoma kitabu hiki, ya kwamba wenye kufanya kazi hiyo wamejaribu sana kutafsiri Neno la Mungu katika lugha itakayowaelea wote.Wala isidhaniwe kabisa kwamba katika tafsiri hii kuna mageuzi yo yote yaliyofanywa ya Neno la Mungu.Hasha!Jambo hilo haliwezekani kabisa. Lakini, na tukumbuke ya kwamba Neno la Mungu halikuandikwa kwanza kwa lugha ya Kiingereza, wala ya Kiswahili.Roho Mtakatifu aliwavuvia watu watakatifu wa kale, Wayahudi na Wakristo,ili kudhihirisha na kutangaza Neno la Mungu. Hao Wayahudi wakatuandikia Neno hilo kwa lugha ya Kiebrania, katika Agano la Kale, tena hao Wakristo wakaliandika kwa Kiyunani, katika Agano Jipya. Basi watu wanaotafsiri Biblia katika lugha za sasa, kwanza huangalia kwa kutunza sana maneno hayo ya asili yaliyoandikwa zamani kwa lugha ya Kiebrania na Kiyunani; kisha wakajaribu kuandika tafsiri iliyo halisi. Mara kwa mara inawezekana kutengeza kidogo hizo tafsiri zilizotangulia kufasiriwa, nasi tumejaribu kufanya hivi, pamoja na kuungamanisha hizo tafsiri za kale.
-
BIBLIA (Medium-Size)
11,500.00FrDIBAJI
Tafsiri hii mpya ya Kiswahili imefanyika kwa ushirikiano wa makanisa ya Kikristo,Wakatoliki kwa Waprotestanti, pamoja na Vyama vya Biblia.
Hii tafsiri ya pamoja ilianzishwa katika mwaka wa 1973, wakati ambapo Wakristo wengi wa Afrika Mashariki ambao Kiswahili ni lugha yao ya mawasiliano, walikwisha kuwa na hamu kubwa ya kuwa na tafsiri ya Biblia kwa Kiswahili chenye kueleweka vizuri zaidi kadiri ya matumizi ya msamiati wa sasa wa lugha yao. Ndiyo maana makanisa yakavitaka Vyama vya Biblia na Muungano wa Vyama vya Biblia vishughulikie jambo hilo.
Mojawapo ya mambo ya kimsingi yaliyozingatiwa katika tafsiri hii ni kwamba Mungu huongea na watu akitumia lugha yao wenyewe na msamiati uleule wanaoutumia wakati huo katika mawasiliano yao. Hali kadhalika,Mungu anapoongea nasi atatumia msamiati wa Kiswahili tunaoutumia sisi wenyewe. Hangetumia Kiswahili kilichoyumbishwa na Kigiriki au Kiebrania kama zilivyo tafsiri za neno kwa neno badala ya maana kwa maana.
Shabaha ya tafsiri hii siyo kuchukua nafasi ya tafsiri nyingine yoyote ya zamani ya Kiswahili. Shabaha yake ni kuwapatia watu tafsiri aminifu iliyo wazi na ambayo imetia maanani mapato ya kitaalamu ya siku za karibuni juu ya lugha ya Kigiriki (AJ) na Kiebrania au Kiaramu (AK) kama zilivyotumiwa nyakati za maandishi hayo; tafsiri iliyo katika muundo wa matumizi ya kila siku ya lugha ya Kiswahili nyakati hizi zetu.
Makala zilizotumiwa kutoa tafsiri hii ni Biblia Hebraica Stuttgartensia,1987,kwa Agano la Kale; na kwa Agano Jipya ni The Greek New Testament,iliyochapishwa na Muungano wa Vyama vya Biblia (toleo la 3 mwaka 1975).Miswada ya tafsiri hii ilipelekwa kuhakikiwa na kusahihishwa na Kamati ya Uchunguzi wa Maandishi ambayo wajumbe wake, wataalamu kwa fani zao zinazohusika katika kazi ya namna hii, walikuwa wa makanisa mbalimbali.Nakala hizo pia zilipelekwa kwa viongozi wa makanisa, vyuo vya filosofia na theologia katika Kenya na Tanzania.
Wote waliohusika kwa mali na hali au kwa namna nyingine katika mradi huu tunawatakia baraka za Mwenyezi-Mungu.
Ilani kwa Msomaji: Maneno yaliyotiwa katika mibano mraba […]yanafikiriwa kuwa hayapatikani katika nakala zote za awali za Maandiko Matakatifu. -
Creative Bible Journal – Girls
6,000.00FrEmbark on an enriching spiritual adventure with the “Creative Bible Journal,” segmented into 8 enlightening parts, each featuring 5 devotions. Designed meticulously, this journal serves as a beacon to guide readers through a threefold growth path: blossoming in knowledge, gratitude, and appreciation towards God; flourishing personally in trust, courage, and strength; and finally, thriving in action by emulating Jesus and crafting a better future.
Tween readers (ages 8-12) will dive into a vibrant world where they can read, ponder, illustrate, and solve puzzles, intertwining faith and creativity to deepen their understanding of the Bible and nurture their faith.
-
Easy to Read Bible
9,000.00FrNavigate through the timeless tales of the Bible with the “Easy to Read Bible,” specially crafted to weave simple words into profound stories, serving as a dual tool for beginner readers to hone their skills while exploring sacred narratives.
Ideal for budding readers, this 208-page children’s Bible doesn’t merely stand as a book but evolves into a pocket-friendly investment, promising to ignite curiosity without being heavy on the pocket. Its reader-friendly text ensures swift and effortless translation, bridging languages and hearts alike.
-
-
-
-
Good News Translation (GNT_Protestant-Edition)
13,000.00FrThe-good-news-translation-gnt-protestant
-
-